Pages

Mtalii alietekwa nyara Kenya amepelekwa Somalia

Serikali ya Kenya inasema mwanamke kutoka Ufaransa aliyetekwa nyara jana usiku, kutoka eneo la watalii Lamu amepelekwa Somalia.

Wamesema kuwa waliomshambulia walikimbia baada ya mapambano ya risasi, wakati walinzi wa mwambao na helikopta kuwaandama na kuwafikia wakiwa kwenye mashua ambamo wamembeba mtalii huyo. Watekaji nyara kadha walijeruhiwa katika mapambano hayo.

Mwanamke huyo, akiwa na umri wa zaidi ya miaka 60 na mlemavu, alikuwa akikaa katika eneo la watalii karibu na Lamu.

Ufaransa sasa imewaonya watalii wasizuru eneo hilo. Majuma matatu yaliyopita, kaskazini zaidi kwenye mwambao wa Kenya, mwanamke kutoka Uingereza alitekwa nyara na washambuliaji kutoka Somalia, ambao walimpiga risasi mumewe na kumuuwa.