Pages

MBUNGE MWINGINE AFARIKI DUNIA


TAARIFA ya iliyotufikia hivi punde katika inaeleza kuwa mbunge wa jimbo la ARUMERU kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Jeremia Sumari (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mh. Jeremia Sumari ni Mbunge wa pili kufariki dunia kwa mwaka huu 2012 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutanguliwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro,Marehemu Regia Mtema aliyezikwa nyumbani kwao Ifakara Mkoani Morogoro jana na mazishi yake yaliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete.

Blogu hii inaendelea kufuatilia taratibu zote za msiba huu na tutaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Mungu ailaze roho za marehemu mahala pema peponi

-Amen


source: http://mrokim.blogspot.com/2012/01/mbunge-mwingine-afariki-dunia-leoni.html