Pages

MZAHA WA VAZI LA TAIFA KUTOKANA NA BENDERA YA TAIFA?

Ni jambo lisilopingika kua kila nchi ina bendera yake, bendera ambayo huwakilisha nchi hiyo katika masula mbalimbali ya kimataifa. kuna symbols nyingi sana ambazo huwakilisha nchi husika, kama nchi. Lakini pia kuna yale mambo ambayo huwakilisha tamaduni na desturi za watu wanaoishi katika hizo nchi.

Ni uelewa wangu kwamba mchakato wa kutafuta vazi la taifa umeanza rasmi, kwa mara nyingine tena.  Vazi hili litakua mahsusi kwaajili ya kutambulisha utamaduni wa mtanzania popote pale duniani. Kamati/Tume iliyoundwa kutengeneza vazi hili imeamua "Kutumia rangi za bendera ya taifa" katika mchakato mzima wa kutengeneza vazi hili. 

Kwa mtazamo wangu huu ni utani usiochekesha. Imagine vazi lenye rangi za njano, kijani,blue na nyeusi??? maswali ya kujiuliza ni kwamba ni nchi ngapi ambazo zinatumia rangi zinazoendana na na za bendera yetu? Na je ni nchi ngapi za kiafrika tunazozijua ambazo kiukweli zina mavazi ya taifa yaliyotokana na bendera ya nchi zao? na je ujumbe ambao vazi la taifa linatakiwa kufikisha utafika kwa kutumia rangi za bendera ya taifa? na mwisho kabisa swali la muhimu ni kwamba msafara wa kitaifa ambao umepembwa na bendera za taifa zinazopepea na zingine zilizovaliwa utaonekanaje?

Suala lilijitokeza hapa ni watu kukosa ubunifu. Samahani kwa nitakaowakwaza lakini mtazamo wangu ni kwamba nchi hii ina makabila mengi sana yenye tamaduni nzuri sana ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kuchangia katika uppatikanaji wa vazi la taifa, zaidi ya hayo nchi ina rasilimali nyingi sana amabazo kitambaa cha vazi la taifa kinaweza kutumika kufikisha ujumbe huo kwa jamii za kimataifa, kuliko kutumia bendera ambayo tayari inajulikana.

Kuazia utamaduni wa shanga za wazaramo, kaniki za wamakonde , rubega za wamasai, shanga za miguu za waha na na makabila mengine yoote yenye mavazi ya asili, tumeshindwa kweli kujumuisha tamaduni hizi na kupata tamaduni moja itakayotuunganisha watanzania wote hadi tunaamua kutumia rangi za bendera?  Mzaha huu, sijauelewa kabisa

Huu ni mtazamo wangu waungwana, msijenge chuki