Pages

ELIZABETH MICHAEL "AKA LULU" AMEMUUA KANUMBA?

Nimejaribu kutafakari suala zima la huyu binti kuhusishwa na kifo cha Kanumba na kwakweli bado sijaweza kuelewa sawa sawa kilichotokea. Nilikua nampenda sana Kanumba, na ni mmoja katika wasanii wachache wa Bongo movies ambae waliweza kunishawishi kuangalia kazi zao kutokana na umahiri wake (hii ni kweli sio sifa za marehemu) lakini suala la kwamba Lulu amemuua Kanumba kwa kusudia mi nakataa kabisa.

Sababu ya kwanza ni kutokana na ripoti za awali kwamba mwili wa marehemu Kanumba haukukutwa na majeraha yeyote yanayoonyeshwa kupigwa kwa namna yeyote ile, however taarifa za hapa na pale zinasema wazi kwamba lulu amekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili ikionyesha kwamba alikua amepigwa (most likely na Kanumba)

Taarifa za Majirani kuhusiana na kusikia kelele za mivutano ndani ya nyumba ya Kanumba muda mfupi kabla ya kifo chake na the fact that Kanumba hajakutwa na majeraha lakini Lulu amekutwa nao inaonyesha dhahiri kuwa Lulu alikua anapigwa na Kanumba.

Taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kua marehemu alikua amekunywa whiskey kidogo kabla ya kifo chake. Kama taarifa hizi ni za kweli basi kiwango chochote cha alcohol kilicho ndani ya damu huweza ku-accelerate kuvuja kwa damu na mengineyo. Hivyo basi kitendo cha Kanumba kuangukana kugonga kichwa akiwa na kiwango chochote cha alcohol kinaweza kuhesabika pia kama chanzo cha hiyo accelerated brain concussion madaktari wanayosema

Tuje basi kwenye body structure na fitness, Kanumba ni mtu ambae alikua anafanya mazoezi ya mwili, nakumbuka kusoma kwenye blog yake kwamba alikua anajitahidi kuwa fit kupunguza kitambi, kwa mantiki hiyo basi kama kweli Lulu amemuua Kanumba basi lazima awe alimvizia kwa nyuma na kitendo ambacho post-mortem report itaonyesha bila shaka. 

Mimi binafsi nasema kwamba kwa mtazamo wangu kama tunataka kumuhukumu Lulu kuwa amemuua Kanumba basi lazima iwe  kwa Sumu na si vinginevyo, manake hata kama kweli Lulu alimsukuma Kanumba katika harakati za kujitetea wakati anapigwa still hiyo sio Murder, ni "self- defence" thats only if kweli alimsukuma.

 Kama hakugusana nae lazima facts kama mazingira ya nyumba (ikiwemo utelezi wa sakafu, kama kweli marehemu alikua ametoka bafuni kama inavyosemekana basi lazima alikua wet na sakafu ya chumbani ilikua wet). Na pia tuangalie kiwango cha alcohol kilichokua kwenye damu na namna kilivyochangia kuzidisha jeraha alilolipata kutokana na kuanguka.

Ni kweli kwamba Lulu ni mtu wa skendo nyingi na anafanya mambo mengi yaliyomzidi umri lakini tusimuhukumu kutokana na hayo. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. kama kweli huyu binti ammemmua Kanumba kwa makusudi basi haki itendeke. Lakini kama hajamuua basi tusimtupie mzigo usiokua wake jamani.


NAMNA ILIVYOTOKEA MPAKA KIFO KILIPOMPATA "HEARSAY"

Kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wa Steve:Marehem alirudi nyumbani na Lulu(usiku),Wakaingia ndani,Kanumba aliingia bafuni kuoga,wakati yupo bafuni Lulu alipigiwa sim alipokea sim akawa anaongea na mtu ambae Steve alihisi ni bwana wa Lulu.



Akiwa bafuni kanumba aliyaskia maongezi yao akatoka akiwa na taulo,aligombana sana lulu,alimpiga,Lulu alikimbia baada ya kuona hali si shwari,Kanumba alimfata hadi nje akamrudisha ndani…akiwa anajitetea baada ya kuona analemewa alimsukuma Steve ili atoke,Steve akawa amejigongA kisogo ukutani.Alidondoka na hakuinuka tena hapo mpaka doctor alipo kuja pronounce kwamba amefariki


"Not every rebelling teenager is famous, if they were trust me You would not have been able to stand your own daughters and sons, so stop pointing fingers"


























HUYU NDIYE ELIZABETH MICHAEL AU “LULU” ALIYEKUWA NA MAREHEUMU STEVEN KANUMBA