Pages

YALIYOMKUTA ULIMBOKA


Dr. Steven Ulimboka (Chini pichani) alitekwa nyara Juzi na watu wasiojulikana na kisha kumpiga sana huku wakimtishia kumuua kwa sindano ya sumu. Chanzo cha karibu na Dr. Ulimboka kinasema kwamba, baada kumpiga sana watu hao wasiojulikana walimtupa msitu wa mabwepande wakiwa wamemfunga mikono na miguu ilhali akiwa uchi wa mnyama kabisa.

Alipozinduka mida yaa saa kumi alfajiri Dr. Ulimboka alijikuta akiwa porini huko, akiwa uchi huku akiwa amefungwa mikono na miguu, alijitahidi akafanikiwa kuifungua miguu yake halafu akaanza kutembea na kwa makadirio ayake alitembea kama muda wa saa moja ndipo alipoanza kusikia sauti za magari yakipita akajua kua yuko karibu na barabara. Hatimae akakutana na msamaria mwema mmoja aliemsaidia kumfungua mikono, na kisha akasimamisha lifti ya gari aina ya starlet ambapo mwenye gari hiyo alibidi arudi nyumba kumtafutia Dr. Ulimboka nguo za kuvaa kabla ya kumkimbiza hospitali ya Muhimbili.

Chanzo changu kimenitaarifu kuwa Dr. Ulimboka anapewa Ulinzi wa hali ya juu na madaktari wenzake wakisaidiana na wauguzi wa hospitali ya muhimbili, na kwa sasa ni watu wachache sana wenye ruhusa ya kumuona.

Awali baada ya kupotea kwake taarifa zilisambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, hadi kupelekea kukamatwa kwake.

Hali ya Dr. Ulimboka baada ya kuokotwa

Hivi ninavyoaandika yupo ICU akiwa katika hali mbaya hajitambui.Awali katikamaelezo yake alisema kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.