Pages

VITUKO DUNIANI: Baba auza mwanae

Polisi nchini Uchina wanamsaka mtu mmoja ambaye aliamua kumuuza mtoto wake wa kiume, baada ya kugombana na mke wake. 
Mtoto huyo aliuzwa kwa dola elfu tano. Kwa mujibu wa BBC mke wa bwana huyo anayefanya katika mji mwingine alianza kumkabili mume wake huyo ambaye ni mvivu na asiyependa kufanya kazi. Bwana huyo alimsubiri mkewe aende kazini na kisha kumchukua mtoto wao na kumuuza kwa familia nyingine. Mama wa mtoto huyo aligundua kuwa mwanaye ameuzwa aliporejea miezi kadhaa baadaye.

Mama huyo alimtafuta mwanae na kumpata, ingawa familia iliyomnunua mtoto awali iligoma kumrejesha kwa madai kuwa walikuwa wametia saini mkataba wa mauzo. Hatimaye familia hiyo ilikubali kumrejesha mtoto huyo baada ya kurudishiwa dola zao elfu tano. Baba wa mtoto huyo amekimbilia mafichoni.

Familia zilizohusika na sakata hilo zimegoma kuzungumza na waandishi wa habari. Polisi pia wamekataa kusema lolote, na mwandishi wa BBC aliambiwa na polisi hao-- Usitangaze kisa hiki, kitatoa picha mbaya ya Uchina-- amenukuliwa polisi mmoja akisema.


PAKA NDANI YA FRIJI

Bwana mmoja nchini New Zealand amekutwa akiishi na paka wapatao sitini nyumbani kwani. Hata hivyo kwa sasa anakabiliwa mashataka ya kutesa wanyama, baada ya paka wengine wapatao 38 kukutwa wamekufa na kuhifadhiwa ndani ya friji lake.

Bwana huyo Donald Cruickshank mwenye umri wa miaka 77, anadaiwa kuhifadhi mizoga paka hao kwa kuifunga na vipande vya magazeti, na kuweka karibu na sehemu anayoweka chakula chake, ndani ya friji.
Shirika la dhamana ya wanyama SPCA limesema maafisa wake walikuta paka 19 wakirandaranda ndani ya nyumba ya bwana huyo, wengine 17 walikuwa wamefungiwa, na paka wengine 23 wakiwa katika ghorofa la chini katika hali mbaya ya kiafya.

Bwana huyo, ambaye amekana mashtaka yake ameliambia gazeti la Herald kuwa aliwahifadhi paka hao ndani ya freezer lake kwa takriban miaka mitatu, kwa sababu hakuwa na muda wa kuwazika.