Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

Mbunge anapofikishwa kizimbani kwa kupokea rushwa


Kweli, hii ni nchi ya kitu kidogo. Ni ukweli usiopingika kwamba rushwa imeenea karibia kila kona ya nchi, tena zaidi sana kwenye asasi zote za serikali. Watu hawaoni haya tena kudai rushwa, tena wanaidai kanakwamba ni haki yao kupewa.  Ila inapokua kwamba watu hao wanaoomba rushwa ni watu waliopewa dhamana na wananchi wa nchi hii ili  kuwatetea maslahi yao na kua sauti yao n jambo la kusikitisha na ni usaliti wa hali ya juu kwa wananchi waliwachagua na kuwapa amana hiyo watu hao.

Nimesikia taarifa kwamba Mbunge wa Bahi (CCM) Omar Ahmed Badwel (43) amekamatwa akiwa anaomba rushwa ya shilingi milioni moja. Sasa basi, mimi huwa sipendi kumuhukumu mtu bila kuufahamu ukweli wote wa mambo, hivyo basi sitasema mengi kuhusiana na suala hili. Lakini, mheshimiwa huyu na wengineo wote kama kweli mnayafanya haya mjijue tu kwamba ninyi ni "wasaliti" na damu za wananchi wenu waliowachagua wanaokufa kila siku kwa kukosa huduma bora za kijamii zimo mikononi mwenu.There is no running away from the truth.



 MBUNGE wa  jimbo la Bahi Mkoani Dodoma  (CCM) Omar Ahmed Badwel (43) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam  leo  kwa tuhuma za kupokea rushwa kiasicha  Mil1 . 


Hapa Mbunge huyo akiwa chini ya ulinzi.(Picha kwa hisani ya Francis Dande).