Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

KICHAA WA BUGURUNI ANAESAFISHA VIOO NA WATOTO WA UBUNGO WASAFISHA VIOO NI KERO KWA WENYE MAGARI

Kwa kipindi cha karibia miezi sita sasa nimekua nikimuona jamaa mmoja mtu mzima tu (kati ya miaka 30 - 40) ambae anaonekana kama mtu mwenye matatizo ya akili pale karibia na mataa ya buguruni. Jamaa huyu huwa anapita kuomba fedha kwenye magari huku mara chache chache akisafisha vioo vya magari ya watu bila kuruhusiwa na kuwadai malipo kwa kutumia nguvu.

Niliwahi kusikia kwamba jamaa huyu huwafanyia fujo watu wanaokataa kumlipa na hata kufikia hatua ya kuwaharibia magari yao lakini nilikua siamini. Lakini leo hii nimemshuhudia jamaa huyu akiwafanyia kitendo cha uchokozi wa hali ya juu wadada wawili waliokua kwenye gari ndogo aina ya saloon rangi ya silver. Hali ilikua hivi;

Jamaa kama kawaida alifika akataka kuanza kusafisha kioo ambacho kilikua kisafi kabisa, dada aliekua kwenye siti ya abiria akamkataza asisafishe, lakini jamaa akatumia mabavu akafutafuta kioo kile, baada ya kumaliza zoezi lake jamaa yule akaanza kudai hela ambapo wale wadada wakamwonyeshea ishara ya kwamba wao hawana hela. Alichokifanya baada ya hapo kichaa huyo ilikua ni kupanda juu ya boneti ya gari, akainua wipers za gari ile na kuanza kuzivunja, akafanikiwa kuzikunjakunja zote mbili halafu akashuka akaishia zake. Wadada wa watu wakabaki hawana la kufanya wakaendelea kuendesha gari yao kuelkea mitaa ya Tazara huku wipers zikiwa zimekunjwa kunjwa.

Hili suala limeniuma sana, kwanza kwasababu mimi ninaamini mtu huyu sio kichaa manake ukimuangalia unaona kabisa kwamba anaelewa fika anavyovifanya, na pia pale buguruni mataa kuna askari polisi wengi sana ambao kwa kipindi chote hiki wamemwachia huyu bwana aendelee kunyanyasa wenye magari, kwa kuwalazamisha wampe hela la sivyo anaharibu magari yao. Huu ni wizi na unyang'anyi wa mchana mchana.

Na kuna suala lingine pia la watoto wanaosafisha vioo barabarani, haswa wale wa taa za ubungo. Wanavamia tu na kuanza kusafisha gari za watu, tena kwa maji yenye sabuni, na wanapokudai hela unapowaonyesha kwamba huna fedha mara nyingi huchanganya tope na maji na kulimwagia gari lako.

 Hii hali inakera jamani, vyombo husika vichukulie hatua suala hili, manake mtu anaamka nyumbani kwake na hasira na msongo wa mawazo kichwani halafu anakuja kukutana na watu wanomlazimisha awape hela ambazo sometimes unakuta kweli mtu hana, mtu unawezakujikuta umeumiza mtu vibaya kweli. kwa usawa huu mtu anaanza kukuingiza hasara za ajabu ajabu za kutengeneza gari bila sababu yeyote ya msingi.

Mamlaka husika mliangalie hili jamani.