Hili ni wazo langu tete,
Katika miaka ya karibuni kumekua na wimbi kubwa la kuongezeka kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini. Nia na madhuni makubwa ya serikali kuruhusu wageni hawa kupewa vibali vya kufanya kazi hapa nchni ilikua ni kuona kwamba ujuzi wao waliokuja nao unafundishwa kwa watanzania ambao hatimae watakua na uwezo wa kufanya kazi hizo zinazofanywa na wageni hao.
Wageni waliokua wanatakiwa kupewa vibali ni watu ambao wana ujuzi wa hali ya juu amabao baadae utakua na faida kwa nchi yetu, na pia nina amini kwamba wageni hawa walikua wana limit ya muda wanaoruhusiwa kukaa nchini, muda ambao utakua umetosha kufundisha watanzania ujuzi ule na kisha kwenda zao kwao.
Sasa basi, sababu zinazonifanya mimi niseme kwamba idara ya uhamiaji inachangia sisi watanzania kunyonywa ni hizi;-
1. Wageni wanaoingia siku hizi wengi wao hawana ujuzi wowote wa ajabu , wengi wao wanaingia na qualifications ambazo watanzania wa kawaida wanazo, tena wengi sana na wapo mtaani hawana kazi. Na wageni hawa wanapofika makazini hupewa huduma zote bure zikiwemo afya, makazi, usafiri, na hadi ada za watoto, zaidi ya hayo wageni hawa wanalipwa kwa dola za kimarekani na mishahara yao yote huanzia dola $1000 hadi $10,000.
Kwanini idara ya uhamiaji iruhusu kampuni iingize accountant kutoka nje? ilhali kuna graduates hadi wa masters wa mambo hayo hayo ya uhasibu na wako mtaani hawana kazi?
2. Mishahara wanayolipwa watanzania tena wenye qualifications zinazowazidi hawa wageni inatia huruma, yani unakuta mtanzania mwenye expirience kabisa na elimu yake ya kutosha mshahara wake haufiki Tsh. 900,000/= . na mshahara huu unakuja mkavu bila beneft ya aina yeyote nyingine. Hii ni haki kweli?
3. Na la mwisho na kubwa zaidi ni kwamba wageni hawa HAWAONDOKI! yani kuna wageni ambao permits zao zinakua - renewed kila zinapoisha kwa karibia miaka ishirini sasa. hivi sisi hatujifunzi tu kutoka kwao? yani miaka kumi, ishirini kweli hakuna mtanzania hata mmoja ambae anakua ameweza kumaster kazi hizo zinazofanywa na hawa expatriates? mbaya zaidi ni kwamba watu hawa matumizi yao yote makubwa huenda kuyafanya makwao wanapoenda likizo, hivyo basi watanzania hakuna hata moja tunalofaidika nalo kwa kuwalipa mishahara hii mikubwa.
Hapo bado hatujazungumzia jinsi wanavyowatreat watanzania wanaofanya kazi kwenye taasisi ama viwanda vyao, hii sio haki hata kidogo na jambo hili linatakwa liangaliwe mara moja na kushughulikiwa.
Taasisi zenye huu mtindo wa kuajiri hadi wapaka rangi kutoka nje ni pamoja na mashirika yote yasiyo ya kiserekali (NGOs) tena haswa zile za kimataifa mi mi staki kutajana majina. Makampuni yote yanayomilikiwa na watu wenye asili ya kiasia (India na China) ndiyo yanaongoza kw kuajiri watu kutoka nje. Tena nje ya idadi inayoruhusiwa kisheria.
Maswali yangu mimi ni je inakuaje mtu anakaa nchini kwetu kwa miaka kumi na zaidi?
Kwanini hamna bodi inayoangalia mishahara ya wafanyakazi wote tu kwa ujumla kuhakikisha kwamba watu wenye ujuzi na ufanisi sawa wanalipwa mishahara sawa bila kuangalia utaifa wao?
Na je inakuaje makampuni yanazidisha idadi ya wageni iliyowekwa na serikali?
Na mwisho kabisa inakuaje mtu ambae hana ujuzi wowote wa ajabu ambao nchini kwetu haupo anapata kibali cha kufanya kazi nchini?
Swali la mwisho la muhimu kabisa ni kwamba Je mapato yao haya yote yanalipiwa kodi????????? wahusika tafadhalini hebu pitieni hizi ofisi na mashirika mjionee mambo. wachache wanakula na wanafaidi lakini athari wanayowaletea watanzania haielezeki.
Hii ni kwa niaba ya watanzania wote wenye ujuzi ambao mpo mtaani kwa kukosa kazi.