Wapendwa,
Kwa wale wote mliopita katika shule hii, kwa namna moja au nyingine hapa mahali pamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuwa watu tulio leo. Hii shule ilianzishwa kwa nguvu za walutheran wa Tanzania, na mimi kama mmoja wa watu waliopita hapa, nakubali kabisa kwamba tuna jukumu la kupaendeleza mahali hapa, pawe mahali ambapo watoto wetu na wajukuu wetu watasoma kwa raha. Natumaini kwa nguvu zetu zote tutaweza kufanikisha kuchangia harambee ya maendeleo ya KLJS katika mwaka huu ambao shule yetu inaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wanafunzi tuliowahi kupita hapa tunapatikana kwenye page ya Facebook inaitwa KILUJUSE tafadhali ingia humu na toa mchango wako wa mawazo. Kamati ya alumni ya KILUJUSE inaandaa tarehe ya kikao cha pamoja, tafadhalini sana kwa wale wote ambao tupo hapa mjini tuguswe kufika siku hiyo. Na kwa wale walioko nje ya nchi na nje ya mkoa tutawaeleza ni jinsi gani mtaweza kuchangia katika tukio hili la kihistoria.
Mungu awabariki sana na awaongezee maradufu pale mtakapotoa.
|
Karibu KILUJUSE - some of greatest people in this country originates here |
|
early volunteers teams, our friends in Christ who helped us build our school |
|
KILUJUSE pioneers |
|
Nathan and other former students |
|
some of the early students |
|
Ngowo, Ezra, Khamsin Babu na Mr Adam, na huyo mzungu ni pastor Wolf? not sure msaada jamani |
|
Anna Mgelwa na classmates, enzi hizo wakiwa njuka - hii ilikua siku ya Pamba na wali bila shaka |