Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

Serikali kulipa madeni yote ATCL

Hivi hizi hela from the beginning alikula nani? na sasa hivi serikali inabidi kutumia hela za walipa kodi kulipia madeni haya? Yani huu ni sawa na uharamia tu, tunapitwa hadi Rwanda kwa kua na shirika la ndege ambalo ni reliable Nchi ambayo juzi tu nusu ya raia wake waliku nchini mwetu?


Serikali kulipa madeni yote ATCL
SERIKALI imeahidi kuendelea kuisaidia Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa kulipa madeni yake yote baada ya kuyahakiki ili kuipunguzia mzigo kampuni hiyo.

Sambamba na hilo, imeipongeza kampuni hiyo kwa kupata cheti cha kuruka (AOC) baada ya kutekeleza masharti yote waliyopewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa ATCL na mpango wa biashara jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

“Nawapongeza kwa kupata cheti cha kuruka, hii ni fursa kubwa kwa Watanzania kuanza kupata huduma za uhakika za kampuni yao na naamini mambo yatakwenda vizuri. Nawatakia mafanikio mema katika mipango yenu mipya,” alisema Naibu Waziri.

Alisema Serikali itaendelea na juhudi zake za kutafuta mbia kwa kampuni hiyo kwani bila kuwa na shirika lenye uwezo wa kutosha kuwaleta watalii nchini, nia ya Serikali ya kutaka ATCL ichangie, Pato la Taifa haitatimia.

Alisema katika mwaka wa fedha uliopita, Serikali ilitenga Sh bilioni 16.7 na itaendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi wa ATCL. Alisema pamoja na kutafuta mbia, Serikali itaendelea kuwashawishi wawekezaji binafsi kuja kuwekeza katika usafiri wa anga nchini.

“Tutaendelea kuruhusu uanzishwaji wa mashirika binafsi ya ndege na mashirika kama hayo yatatambulika kama mashirika ya Tanzania na Serikali itayapa haki za kutoa huduma ndani na nje ya nchi ili usafiri wa anga uwe wa ushindani hivyo kutoa unafuu kwa watumiaji wake,” alisema.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Paul Chizi alisema ATCL itahakikisha inakwenda na utaratibu endelevu ili kuhakikisha AOC yao haishuki kama ilivyowahi kutokea na wakazuiwa kufanya safari zake.

“Mwaka 2008, ATCL haikukidhi hadhi ya kuwa na AOC ndege zake zikawa zinaruka kwa masharti na hawakuruhusiwa kabisa kufanya safari za nje, lakini sasa tumepata kibali cha kuruka bila mashari yoyote na tumejipanga kuhakikisha hadhi ya shirika inapanda,” alisema na kuongeza kuwa mambo yakienda vizuri, ndege zake zitaanza safari za Dar es Salaam Kigoma na Tabora kabla ya kuisha kwa mwezi huu.





http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=22137