Get Paid To Promote, Get Paid To Popup, Get Paid Display Banner

WABONGO HII NI AIBU: Butiama waomba maji serikalini

VIONGOZI katika Kata ya Butiama, mkoani Mara wameiomba Serikali iwezeshe upatikanaji wa
maji kutokana na kile kilichoelezwa kwamba eneo hilo linakabiliwa na kero kubwa ya huduma hiyo.

Mtendaji wa Kata ya Butiama, Joseph Mukama aliliambia Habarileo kwamba maji katika kata hiyo hususan kijiji cha Butiama ambako ndiko makazi ya Mama Maria Nyerere, ndoo moja ya
maji huuzwa Sh 300 jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wananchi.

“Kijiji cha Butiama ni sehemu nyeti. Mzee Msuguri na Mama Maria walipaswa kuheshimika. Wakati mwingine ilibidi jeshi lilete maji kwenye magari, ndio maji yameanza kutoka,”alisema
Katibu Tarafa ya Makongoro, Lucy Makenge.

Mtendaji wa Kijiji, Raphael Kakwaya alisema kitendo cha huduma hiyo kukatika baada ya Mwalimu Julius Nyerere kufariki, kinaleta picha mbaya, hali ambayo inaweza kufikiriwa kuwa
serikali haiwajali wananchi wa Butiama.

Kakwaya katika kuelezea pengo aliloliacha Nyerere, alisema enzi za mwalimu huduma zilipatikana bila usumbufu.

“Kwa mfano maji ya bomba yalikuwa ya uhakika lakini sasa maji ni mara mbili na wakati mwingine mnakaa muda mrefu bila kuyapata,” alisema.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa Butiama waliozungumza kwa nyakati tofauti, wamepongeza uamuzi wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kijijini hapo.


http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=21773